GET /api/v0.1/hansard/entries/1358582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1358582,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358582/?format=api",
    "text_counter": 372,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "hata ya siku zake mwezi wa sita mwaka ujao, Decemba hii tayari Serikali ya Kenya italipa Dollar milioni mia tatu. Hilo ni jambo ambalo tunaona Serikali inaendelea kuwa dhabiti. Hii ni kwa sababu hauwezi ukalipa deni ikiwa wewe si dhabiti. Ni vizuri kulipa madeni uliyo nayo. Tayari tulikuwa tumechukua zaidi ya Dollar bilioni mbili. Bw. Spika wa Muda, tulipokuwa tukizunguka Jamhuri ya Kenya tukiomba kura, Rais alisema atazingatia Hustler Fund. Wakati huu tunapoongea, mwezi jana, zaidi ya `Ksh36.8 bilioni zilikuwa zimechukuliwa na wananchi wa Kenya. Hawa ambao tunawaita hustlers ama walala hoi tayari walichukua hela hizi na zimewasaidia kwa shughuli zao za biashara. Vile vile, wameweka akiba ya zaidi ya Ksh2.3 bilioni. Kwa hivyo, napongeza vile Rais alivyotoa Hotuba yake na kulenga mambo ambayo amefanya na mambo yale Serikali inaendelea kufanya. Hakukomea hapo. Kwa mambo ya elimu, Serikali imeajiri zaidi ya walimu 56,000. Hilo ni jambo nzuri ambalo sisi na wanafunzi watajivunia kwa sababu kumekuwa na shida katika nchi yetu ya Kenya. Tangu tupate Uhuru, hakuna wakati walimu wameajiriwa wengi zaidi ya idadi hii. Kwa hivyo, tuna kila sababu ya kumwambia Rais anaendelea vizuri na analenga ndipo, na aendelee vivyo hivyo. Tulipokuwa tukitembea tukiomba kura kwa wananchi wakati wa siasa, shida iliyoko kubwa katika Jamuri yetu ya Kenya na ndio ukweli, ni vijana wetu kukosa ajira. Rais ameleta mfumo wa kujenga nyumba ambazo watu wanaweza kununua. Hizi nyumba zitasaidia vijana wetu. Vijana wetu ndio watakaotengeneza madirisha katika sehemu za jua kali. Vijana wetu ndio watatengeneza milango, ndio wataweka hizi nyumba maji, na kuweka umeme. Hiyo itapatia vijana wetu ajira kwa sababu hawachagui kazi bora wapate pesa. Hizi nyumba zitatengenezwa katika kila sehemu ya nchi ya Kenya hasa kuanzia pale Nanyuki mahali panaitwa Yard, na ninajua hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kenya ataenda kufungua hizi nyumba. Ningependa kuwambia vijana wetu pale Nanyuki na Laikipia wakae chonjo wakingoja. Kazi zitapatikana na tutafanya zile kazi. Kwa hivyo, nina kila sababu ya kuunga mkono Hoja hii ya Hotuba ya Rais. Ni dhahiri shahiri Rais alionekana katika sikukuu iliyopita akizindua hawa wauguzi wa nyanjani. Tayari tuna wale wauguzi. Mimi nilikuwa pale Laikipia wakati Gavana wa Laikipia alikuwa akizindua wale wauguzi wa nyanjani. Kwa hivyo, hawa wauguzi laki moja wapo na tunajua wataendelea kufanya kazi nzuri. Watakuwa tegemeo kwa sababu, nchi isiyo na afya, itakuwa na ukosefu wa watu wanaoweza kufanya kazi. Hivyo basi ni ukweli hao wauguzi laki moja wako chonjo na ngangari na wanaendelea kufanya kazi wanayopaswa kufanya. Jambo lingine Rais alilolisema na ni nzuri zaidi ni hawa vijana wetu wa National Youth Service (NYS). Alisema wakati huu watu watachukuliwa kiasi cha vijana 40,000. Kilichonifurahisha ni Rais kusema kwamba watachukuliwa katika vijiji vyetu. Hakukomea hapo. Aliongeza ya kwamba, baada ya wao kwenda NYS, wakimaliza kusomeshwa wao ndio wakaokuwa wakijiunga kuwa askari polisi baada ya kwenda kwa mafunzo ya askari polisi au askari jeshi. Hivyo basi, katika sehemu zote zetu, vijana wetu watakuwa wameguzwa na hili ni jambo muhimu sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}