GET /api/v0.1/hansard/entries/1358583/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1358583,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1358583/?format=api",
    "text_counter": 373,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Hawa majeshi watapata maarifa. Itawezekana wao ndio watengeneza barabara, kuweka nyumba maji na vile vile kuweka stima kwa sababu watasoma haya mambo. Bw. Spika wa Muda, kuna jambo lingine ambalo alilitaja. Alisema ya kwamba katika nchi ya Kenya kuna shida, kwa sababu tunapata mazao lakini soko zetu si nzuri sana. Alisema vizuri ya kwamba tutakuwa na soko katika sehemu nyingi za nchi yetu ya Kenya na zile soko zitakuwa na stima na maji. Kwa hivyo, ijapokuwa ndugu zangu wa upinzani wanasema ati Hotuba yenyewe haikuwa nzuri, Mswahili husema ‘Mgala muue na haki umpe.’ Kazi nzuri imefanywa. Ukitembea utaona haya maneno yote yakifanyika. Sitakomea hapo, kwa sababu aliongea kuhusu pembejeo. Wakati mwingi unapata iko katika miji zetu tu. Alisema ya kwamba pembejeo zipelekwe mashinani pia. Alisema isipelekwe Nanyuki peke yake, ipelekwe Rumuruti, Salama, Matania, Thome na sehemu ambayo watu wanaweza kupata pembejeo bila kulipa nauli yoyote. Hiyo ndiyo kuinua hali ya maisha ya watu. Bw. Spika wa Muda, kwa wengi ambao wanaongea kuhusu unga, ni vizuri alisema ya kwamba inategemea ni unga upi ambao wewe unatumia. Kwa sababu, wengi ambao wanaongea hapa ni mabwenyenye kulingana na mahali wananunua unga. Hawa si walala hoi. Kwa hivyo, ni vizuri waangalie mahali ambapo Rais alisema. Mimi ningependa kumalizia hapo nikisema ya kwamba naunga mkono na vile ambavyo Rais alisema. Tutaendelea kumuunga mkono ili wananchi wa Kenya waweze kupata afueni. Nashukuru."
}