GET /api/v0.1/hansard/entries/1359075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1359075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1359075/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, UDA",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Spika wa Muda. Ninaungana na wenzangu kuunga mkono Ripoti hii ya Kamati kwa uteuzi wa wajumbe wa kidiplomasia ambao wanaenda kuwakilisha nchi hii kule nje. Wakati ambapo mabalozi huteuliwa, wao huteuliwa kwa dhana ya nchi, ili nchi iweze kufaidika wakati wanaiwakilisha kule nje. Wao pia ni wahusika wakuu kwa kuleta uhusiano mzuri kati ya nchi ambayo iko na nchi hii. Kwa hivyo, ni nafasi nzuri ambayo wamepewa na nchi hii kuiwakilisha ili nchi hii iweze pia kuheshimika kule nje. Tuko na bidhaa nyingi ambazo tunaweza kuuza pale nje. Mabalozi watakaotuwakilisha watakuwa na njia mwafaka kueleza nchi hizo kuhusu mazao yetu mengi ya ukulima. Ni muhimu wajue kuwa tunakuza vitu vingi ambavyo pia tunaweza kuuza kule nje. Wamepewa nafasi muhimu ili waweze kuimarisha uchumi wetu kwa kukuza yale ambayo nchi hii inaweza kuzalisha. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}