GET /api/v0.1/hansard/entries/1359076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1359076,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1359076/?format=api",
"text_counter": 183,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, UDA",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, nchi hii pia imeimarika katika utalii na ni jukumu lao kukuza maeneo ya kitalii katika taifa hili ili tupate watalii wengi watakaoleta fedha za kigeni zitakazoimarisha Shilingi ya Kenya sababu imezorota sana. Tutakapopata watalii wengi nchini, tutaimarisha hela za nchi hii. Tuna wanafunzi wengi ambao wako na maono ya kusoma katika zile nchi za nje. Ni jukumu la hawa mabalozi wakati ambapo wametumwa kule na Serikali kuhakikisha kwamba wanatafuta nafasi nyingi kwa watoto wetu ili waweze kwenda kusoma na pia kupata ajira katika nchi zile. Hawa mabalozi wetu wataweza kuinua jina la taifa hili kwa sababu Rais wa sasa ameimarisha uhusiano wa Taifa la Kenya na nchi zingine. Kwa hivyo, ni jukumu ambalo wanafaa kulichukulia kwa umuhimu sana ili tuweze kupata marafiki wengi watakaoshirikiana na nchi hii. Mhe. Spika wa Muda, ninawapa kongole, na wanapoenda kwenye nchi hizo wafanye kazi vyema. Ninaomba kuunga mkono Ripoti hii. Ahsante sana."
}