GET /api/v0.1/hansard/entries/1359696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1359696,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1359696/?format=api",
"text_counter": 541,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika. Kwa sababu ya umoja wa watu wa Lamu, ninaomba kujibiwa maswali ya pili na tatu kwa maandishi. Nimeshajibiwa swali la kwaza katika vyombo vya habari. Pia, Rais na Waziri Kindiki wamevalia njuga swali letu la kutengwa au marginalisation . Ndio maana tunapata barabara ya kwanza. Rais alikuja kuweka barabara ya kihistoria siku ya Jumamosi. Katika miaka sitini, hatujawahi kupata even one inch ya barabara, lakini Rais alikuja kutuwekea barabara. Waziri Kindiki anang’ang’ana sana na mambo ya marginalisation au jamii zilizotengwa. Hayo yatasaidia katika usalama. Wale wanaotumia kutengwa na kugawanywa kwa watu wa Lamu katika siasa hawataweza kutugawanya tena."
}