GET /api/v0.1/hansard/entries/1360814/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1360814,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1360814/?format=api",
"text_counter": 720,
"type": "speech",
"speaker_name": "Gov. Kawira Mwangaza: “",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kila siku wanamtafutia makosa wanataka Kawira awasaidie kuiba. Kawira akakataa na akasema yeye hataki wizi. Wakati alipokataa walianza kumchimbia mashimo. Wanataka Kawira akule pesa nao. Wanataka Kawira akule pesa za barabara. Wanataka Kawira akubali wakule pesa ya dawa hospitalini. Wanataka Kawira awasaidie kula mali yetu. Igembe nawaeleza kweli kabisa, mpaka sasa sikilizeni kwa makini. Wanapanga pia kuyachukua maisha ya Kawira. Wanapanga sasa kumuua Kawira. Lakini najua kwa maombi yenu huyo shetani ameshindwa katika jina la yesu. Ati walikuwa wanasema tangu ile wakati wa impeachment ya kwanza kuwa Kawira hajawai kunywa chai katika mikahawa ya Kaunti ya Jiji la Nairobi. Mara ya mwisho ya kunywa chai katika mikahawa ya mji wa Nairobi ni ule wakati wa i mpeachment . Hiyo ndiyo inafanya maadui wake wakasirike kabisa. Eti wanamtaka Kawira asiende Okolea aende kule Nairobi wakunywe naye chai kwa pesa zenu. Kawira naye amekataa kata, akasema kazi yake ni mashinani. Wenye wivu wajinyonge. Wenye wivu wajinyonge”"
}