GET /api/v0.1/hansard/entries/1361720/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1361720,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1361720/?format=api",
"text_counter": 1626,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mjadala huu ambao uko mbele ya Senate ni Mjadala ambao tunatakikana tuusikilize halafu tufanye uamuzi. Ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kufurusha kutoka kwa ofisi ama ikiwa hakuna, tuweze kumpatia nafasi ingine aweze kuendelea. Bw. Spika, kama kuna wakati wowote ambao Seneti inatakikana kujitambua na kuweza kuonekana iko kazini na inafanya kazi, ni wakati huu ambao inahusikana na serikali zetu za mashinani. Wakati huu ni wa kujitambua ya kwamba mtu ambaye amefanya makosa anaweza kuchukuliwa hatua ama ambaye amefanya makosa isiyo ya kiwango cha juu, anaweza kupewa nafasi kuendelea. Cha muhimu katika mjadala huu wetu ambao umeletwa katika Kipengele cha 181 cha Katiba na vile vile, katika Kipengele cha 33 katika County Governments Act. Vile vile, kulinganishana na Kanuni zetu za Kudumu za Bunge la Seneti, Kipengele cha 80. Kibarua kilichokuwa hapa jana na leo ni kikubwa sana. Tumeweza kukaa katika hili Bunge letu la Seneti kuanzia mapema na tumefika Saa Sita usiku. Hivi leo, tumeanza asubuhi na mpaka sasa bado tuko hapa. Hili ni jambo ambalo nawapatia kongole Maseneta wote walioko hapa kwa kazi yao nzuri waliyoweza kuifanya kusikiza mjadala huu. Wakenya wote hivi sasa macho yako katika Seneti. Na wanaangalia. Wameweza kujionea katika wale mawakili wazuri na majabali wa sheria kwa upande wa Gavana Mwangaza na wa County Assembly ya Meru. Tumeweza kuwasikiza na tunahakika kwamba Maseneta wataamua mashtaka haya kwa njia inayotakikana kisheria na kulinganishana na Kanuni zetu za Bunge. Bw. Spika, cha muhimu ni kwamba sisi sote ni wazazi. Pengine ningejiunga pamoja na ndugu yangu hapa, Sen. Cheruiyot, aliyesema yeye pia yuko na watoto. Pia mimi niko na watoto wawili wa kike. Cha kwanza sikuweza kufahamu kabisa kwamba kuna picha ambazo zinaweza kuonyeshwa na ukajitafakari wewe mwenyewe. Kama ni mke wako, mama yako, ndugu wako wa kike au mtoto wako wa kike."
}