GET /api/v0.1/hansard/entries/1361804/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1361804,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1361804/?format=api",
    "text_counter": 1710,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Nashukuru kwa nafasi hii ambayo nimepewa kujadili Hoja nzito za usawa, haki na ukweli. Ukipewa nafasi kutafuta amani kati ya wendawazimu wawili, unashidwa utaanza vipi. Iwapo wewe ni mhubiri na unamuombea mwendawazimu, utafumba macho ukiomba ama utayakodoa macho pima ukiomba? Hii ndio hali tumo sasa. Tunakashifu matamshi mabaya dhidi ya wanawake. Lakini pia lazima tukashifu matendo mabaya yanayotendwa na wanawake. Iwapo kuna ubadhirifu wa pesa lazima tuseme. Iwapo kuna matusi dhidi ya wanawake na jinsia zao lazima tukashifu. Iwapo viongozi hawawezi kaa pamoja na kujadiliana lazima tuseme ukweli. Katika jamii yetu tunasema ‘maji yasipotifuliwa hayawezi tulia’. Haya maji ya Meru yametifuliwa na lazima tuwache yatokote na yatulie. Yamefika hapa yakitokota lazima tuamue yatulie na watu wa Meru wasonge mbele. Haiwezekani viongozi hawa kusema yale wanayosema pasipo shinikizo ama kunyoshewa vidole na viongozi wengine. Iwapo wewe ni bishop na unasema ‘wenye wivu wajinyonge,’ ni mahubiri yepi tunaendeleza katika nchi ya Kenya? Lazima tuseme ukweli."
}