GET /api/v0.1/hansard/entries/1361853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1361853,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1361853/?format=api",
    "text_counter": 1759,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "tunasema talaka ni mara tatu. Unaweza kumpa mke talaka akaenda akarudi. Ukampa ya pili, akaenda akarudi. Ya tatu ndio huwa ya mwisho. Kwa hivyo, Gavana Kawira alikuja hapa mara ya kwanza mwaka jana na talaka haikuweza kupita. Kwa hivyo, ako na fursa nyingine kuja hapa kuangalia ni vipi atatatua matatizo yake. Ni masikitiko kwamba ushahidi uliotolewa haukuweza kuthibitisha makosa yaliyodaiwa kufanyika na Gavana Kawira. Ukiangalia makosa yote yaliyozungumziwa hapa na ushahidi uliyoletwa haukuweza kufikia kiwango kilichowekwa na Mahakama ya Upeo katika kuangalia maswala kama haya. Itakuwa ni dhuluma kubwa kuweza kumpeleka nyumbani Gavana Kawira Mwangaza kwa ushahidi ambao haukufikia kiwango kinachohitajika na mahakama. Bw. Spika, uamuzi utakaofanywa usiku wa leo, hautasaidia yale matatizo ambayo yako Meru. Ni jukumu la viongozi ambao walichaguliwa wote, kuhakikisha kwamba tatizo hili wameweza kulitatua wao kama viongozi wa Meru. Hii ni kwa sababu matatizo ya Meru haiwezi kutatuliwa na viongozi wa kutoka Isiolo, Mombasa wala viongozi kutoka sehemu yoyote isipokuwa watu wa Meru wenyewe. Ni, waketi chini, waangalie matatizo haya ili waweze kuamua, ili waweze kupata maendeleo kama ilivyotarajiwa na Katiba yetu ya Mwaka 2010. Kwa hivyo, kwa kumalizia ni kwamba tumepata fursa ya kujua matatizo ya Meru. Fursa hii iko katika kaunti zetu zote tulizonazo katika nchi yetu ya Kenya. Isiwe kwamba, wakitoka hapa mmoja aseme ameshinda. La. Watakaokuwa wameshinda ni watu wa Meru kupata uongozi na viongozi ambao watasaidia kupeleka Kaunti ya Meru mbele. Asante."
}