GET /api/v0.1/hansard/entries/1363709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1363709,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1363709/?format=api",
"text_counter": 310,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii niweze kuunga mkono Hoja hii iliyoko mbele ya Bunge hili, na pia nimpe kongole Mwenyekiti wangu wa Kamati ya Regional Integration, ambaye nilitembea naye pamoja katika haya maeneo ambayo yamezua utata leo hii juu ya ujengaji au uidhinishaji wa kituo kimoja cha kupima mambo ya mizigo na uchukuzi. Kwa kusema ukweli, mimi nimetoka sehemu ya Pwani. Sehemu ile ina sehemu nyingi sana ambazo kuna vizuizi ambavyo ukiangalia haviwezi kujenga na kuweza kulainisha biashara inayotoka sehemu ya Bandari ya Mombasa. Hizi ni sehemu ambazo tukiwa na kituo kimoja cha kuweza kupima mizigo ambayo inaelekea sehemu ya juu ya taifa hili au Uganda, Sudan ya Kusini na mataifa mengine ya Afrika Mashariki, yataweza kulainisha biashara. Hii yote inasababisha usumbufu kwa wafanyibiashara wetu ambao wanatumia sehemu hizi. Jambo jingine ni kwamba katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya, kuna vizuizi vya barabarani visivyo pungua 27, ambavyo ni usumbufu zaidi. Unazuia na kuvunja mioyo ya wafanyibiashara wengi wanaotumia barabara zetu wakiangalia kuwa unasimamishwa bila sababu yoyote, mzigo unaangaliwa, ambapo katika sehemu uliotoka ya kwanza kabisa mahali mzigo ulipakiwa, mzigo ule ulipimwa na kuidhinishwa kusafiri. Lakini unapata kuna usumbufu mwingi katika barabara. Kamati hii ilipokaa baada ya kutembea, ikaonelea kwa nini tusiwe na kituo kimoja cha kuweza kupima, kuidhinisha, kuwezesha, kurahisisha na kulainisha misafara ya kuweza kuelekea sehemu zingine za nchi hii. Nimetoka sehemu moja pale Lunga Lunga. Ukipita pale mpaka wa Kenya na Tanzania, unapata kuna vizuizi vingi barabarani vya kuzuia tu wafanyibiashara wadogo na vijana wetu wa usafiri ule wa daladala au bodaboda. Hii ni mbinu ya ndugu zetu wale wa usalama. Tunajua wanachunga usalama na wanafanya kazi nzuri, lakini sasa ikifika kusumbua wale wanaosafari au wanaosafirisha mizigo bila sababu yoyote, unapata mtu anasimamishwa mara tatu, nne au tano, mpaka unakuta ule mzigo alioubeba unapoteza dhamani yake. Kulainisha sheria ya kuwa mzigo ukitoka kwa kaunti ile ambao umetokea ama imetengenezewa pale, mbona kusiwe na sheria ya kuwa hio kaunti pekee yake ndio inawewa kutoza ushuru? Unapata mzigo umetoka sehemu ya Lunga Lunga, unakuja mpaka mahali inaitwa checkpoint, analipa. Anatoka, hata kilomita mbili ni nyingi, unapata tena mzigo unalipishwa tena ushuru mwingine na watu wa Kaunti ya Mombasa. Ukisonga tena kidogo ukifika Mariakani, pia utalipa ushuru. Kamati hii ikaona huo ni usumbufu kwa Wakenya, na sisi tuko hapa kulinda masilahi ya Wakenya wetu wanaofanya biashara na kusafiri. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}