GET /api/v0.1/hansard/entries/1363763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1363763,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1363763/?format=api",
    "text_counter": 364,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kirinyaga County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Njeri Maina",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii. Hata ninamskia Mhe. Muhia akicheka kwa kunisikia nikizungumza lugha ya Kiswahili. Mhe. Spika wa Muda, ninakumbuka nilipokuja katika hili Bunge mara ya kwanza, niliweza kuchanganya lugha ya Kiswahili na lugha ya Kimombo. Nilirekebishwa na kuambiwa kuwa hatufanyi hivyo. Ninakumbuka kuwa niliona watu kwenye mitandao wakinukuu MaidenSpeech ya Kirinyaga Woman Representative. Sasa safari imeanza. Nimekolea kidogo na ninajua kuwa vijana hapa Bungeni wanajikakamua. Ninaiunga mkono Ripoti hii. Ugawaji wa rasilimali ni swala nyeti hapa Kenya."
}