GET /api/v0.1/hansard/entries/1363771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1363771,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1363771/?format=api",
"text_counter": 372,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kirinyaga County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Njeri Maina",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Spika wa Muda, tutamwondoa huyu Mbunge. Ninajua kuwa Mhe. Cynthia Muge ni mtu wa kanisa. Kwa hivyo, ninajua kuwa Mhe. Osoro ataokoka ili atoe fikira zake kwa mambo ambayo sio ya hapa Bungeni. Ninaunga mkono Ripoti ambayo imeletwa hapa na Mhe. wa Molo. Tumekuwa na mazungumzo hapa Bungeni na pia kule nje, tumesikia watu wakisema kuwa tuhakikishe kuwa tunagawa rasilimali za Kenya kulingana na kanuni ya kura moja, mtu mmoja, na shilingi moja. Kuna wale pia wanasema tuongeze kilomita ya mraba moja katika lengo hilo. Ni tatizo wakati kama huu kujua kuwa kuna watu ambao hawafikiri kabisa rasilimali hapa Kenya. Tumekuwa tukihakikisha kuwa tunaandikisha na kujua ni jumla ya watu wangapi ambao wako katika viwango tofauti. Bado kuna watoto ambao wanabaki nyumbani na hawaendi shuleni. Kuna watu katika sekta tofauti tofauti ambao wamesaidiwa na zile fedha ambazo zinapeanwa na hili Bunge kwa usaidizi wa masomo. Lakini kuna sehemu nyingine ambapo watoto wanabaki nyumbani maanake tunagawa rasilimali za hapa Kenya kwa namna ambayo si sawa kabisa. Kuna shule kule Mwea, Kirinyaga County ambayo haina misingi. Hakuna mahali pa watoto kuketi na kuchezea. Hatuwezi kufananisha watoto hao na wale ambao wako katika shule ambazo zina misingi bora. Masomo yao hayawezi kutoshana na masomo ya wale ambao wana rasilimali za kutosha Tunajua kuwa tuna sheria ambazo ziligatua mambo ya afya kwenye..."
}