GET /api/v0.1/hansard/entries/1363773/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1363773,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1363773/?format=api",
"text_counter": 374,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kirinyaga County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Njeri Maina",
"speaker": null,
"content": "… kwenye counties, Mhe Spika wa Muda. Tulipoleta devolution, hatukuhakikisha kuwa tunajua ni watu wangapi mahali fulani ambao wanahitaji dawa. Hakuna dawa katika hospitali zetu kule Kirinyaga County na kwingineko. Kwa hivyo, tukizungumzia hayo maneno, lazima tuhakikishe kila mtu anaweza kujivunia kuwa Mkenya. Vijana wetu wamesoma lakini kazi hazipo. Lazima, kama Bunge, tuhakikishe kuwa tunajua, kwa mfano, ni vijana wangapi wanaoishi hapa Nairobi. Kama ni Kirinyaga County na county zingine… Tunajua kwamba kuna migration, kwa mfano, watu watoke Kirinyaga waje Nairobi. Tunahitaji kujua ni watu wangapi wako Kirinyaga County na tuunde misingi ya kuwawezesha kujikimu kimaisha wakiwa Kirinyaga County ili waweze kujikuza. Ninaunga mkono Hoja hii. Tuhakikishe kuwa tunagawa rasilimali kwa usawa kwa kila Mkenya. Shukrani."
}