GET /api/v0.1/hansard/entries/1367486/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1367486,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1367486/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika. Nashukuru kwa nafasi hii kwamba mhusika mkuu katika mchakato wa kubanduliwa nje ya kiti apewe nafasi hii kujieleza wazi, Wakenya wakisikiza. Vile vile, madai ambayo viongozi wa wadi wako nayo, waje wajieleze na stakabadhi zinazoweza kudhibitishwa na Seneti. Halafu, kama ni kunyolewa, watu waandae maji, sabuni na haki itendeke kwa yeyote ambaye atakuwa na makosa. Iwapo hana makosa, atasamehewa. Ninavyofahamu ni lazima kila mtu awajibike katika uongozi. Tutakuwa tunampa nafasi, yeye na Bunge la Kaunti, ili waaajibike kutokana na hoja watakozoleta Seneti. Gavana na wenzake wawe kielelezo kwa magavana wengine Kenya hii watakaojipata katika hali kama hii. Pia, wawakilishi wadi wa kaunti mbalimbali watakaokuwa na hoja kama hii wakilizileta hapa, wawe wamejiandaa kikamilifu ili tuamue kama Seneti – watu timamu na wanaolinda ugatuzi."
}