GET /api/v0.1/hansard/entries/1367668/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1367668,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1367668/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kuanza na ya kwanza. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu Nambari 53(1) kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Elimu, kuhusu ongezeko la visa vya mimba za mapema kwa wanafunzi wa shule za upili katika Kaunti ya Bungoma. Katika kauli hiyo, Kamati iangazie yafuatayo - (1) Iarifu Seneti kuhusu idadi ya wanafunzi wa shule za upili katika Kaunti ya Bungoma waliopata mimba mwaka huu wa 2023, ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2022. (2) Ibaini sababu zinazopelekea kuongezeka kwa visa hivyo vya mimba za mapema, hususan katika shule ya Upili ya St. Thomas Aquinas, Chesikaki ambapo wanafunzi takriban 54 wameathirika, hii ikiwa ni asilimia 22 ya wanafunzi wote shuleni humo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}