GET /api/v0.1/hansard/entries/1367962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1367962,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1367962/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia maombi ya taarifa kutoka kwa Sen. Okiya Omtatah kuhusiana na kudhaminiwa kwa baadhi ya mashirika ya umma na Serikali kuu. Ni masikitiko kwamba baadhi ya mashirika yanaendelea kupata hasara. Hasara hii inabebwa na wananchi wa kawaida ambao wanalipa kodi kuisaidia Serikali. Hususan Shirika la Kenya Airways ambalo kwa muda mrefu limeweza kutegemea Serikali kulieka hai. Juzi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo amesema kwamba kwa mwaka huu, watapata hasara ya Kshs85 bilioni. Wametoa mapendekezo kwamba mwakani, watapata hasara ya Kshs65 bilioni."
}