GET /api/v0.1/hansard/entries/1368036/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1368036,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1368036/?format=api",
    "text_counter": 216,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Ninasimama kuunga mkono Mswada huu kwa sababu ni mzuri na wasichana ambao wanapata mimba za mapema waweze kutunzwa na kulindwa. Lakini kwa usemi huo huo, ni vizuri ijulikane kuwa mimi sishabiki wala kukubali ya kwamba wanapaswa kutunzwa na kulindwa. Tukifanya hivyo, tutawahimiza wapate mimba za mapema. Ni vizuri ijulikane kuwa katika mila na desturi zetu, haswa sisi, Waafrika, kuna msemo tunaotumia kuwa, “Mtoto amevunjwa mguu”. Jambo hili likifanyika, wazee huwa wanaenda katika ile familia na kufanya mambo ya kidesturi. Ninakubaliana na Mswada huu kwa sababu baada ya wasichana hawa kupata mimba za mapema, wengi wao huwa wanataka kurudi shuleni waendelee na masomo yao. Kwa hivyo, ni vizuri kuunga mkono Mswada huu kwa sababu unaangazia mambo hayo kuwa wasichana wale wanapaswa kupewa fursa ya kurudi na kuendelea na masomo yao ili tusiwanyima human rights zao . Waswahili husema, “kosa si kosa, kurudia kosa ndio kosa.” Kama waliyoongea mbele yangu walisema hawa ni wasichana wadogo, pengine wanafanya mambo haya ya kimapenzi bila kujua na wanajipata katika hali ya sitofahamu. Ni vizuri, wale ambao wako katika taasis za elimu, hasa waalimu wakuu na wale wanaohusika katika mambo ya kuendeleza masomo wawapatie fursa nyingine kwa sababu, wasichana hawa wanaweza kuwa walitenda jambo lile bila kujua. Wanaweza kuwa watu wa manufaa baadaye. Pengine lile lilikuwa kosa la mara ya kwanza. Ukiangalia desturi zetu, utapata kuwa katika sehemu zingine hasa sehemu za Laikipia, wasichana wanaozwa mapema. Kuna mashirika ambayo yanaenda kuwaokoa wasichana wale ambao wameozwa mapema. Ikiwa Mswada kama huu hautapita, tuendelee kuwashughulikia wasichana wale, hatutakuwa tumewasaidia ikiwa tutawaokoa lakini hatuwezi kuwatunza kwa njia ambayo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}