GET /api/v0.1/hansard/entries/1368037/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1368037,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1368037/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "inafaa. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu unahimiza Serikali kuu imakinike na itilie mkazo kuangalia maneno hayo. Mswada huu haukomi pale, unaendelea kusema ya kwamba, gatuzi zetu zinapaswa kuangalia zile sehemu ambazo hawa wasichana ambao wamepata mimba za mapema wanapelekwa. Kifungu cha 11(2) kinasema ya kwamba msichana akishukiwa kuwa na mimba, hawapaswi kushurutishwa kuenda hospitali ama kukaguliwa. Hapa kuna tatizo kwa sababu huyu ni mtoto ambaye hawezi kujifanyia uamuzi. Pengine tungesema ya kwamba ikiwa tayari amemwambia mzazi wake na wameangalia vizuri. Ni jukumu lao kuwa na ule msukumo kwa sababu huyu ni mtoto na hawezi kufanya uamuzi mwafaka. Hata sisi tutakuwa tumefeli katika maelezo na maagizo yetu. Inapaswa kuwe na msukumo hata akiwa ni mtoto mdogo. Ninajua kuwa wale ambao wanahusika na mambo haya watasema kuwa hapaswi kuambiwa moja kwa moja kwa sababu ni mtoto. Hata hivyo, mzazi ama mtu yule ambaye ana uwezo wa kumwambia aende akaangaliwe hospitalini, basi anastahili kufanya hivyo. Tena, mtoto kama huyu akipata shida katika ile shule, yule ambaye atachukuliwa hatua ni mwalimu mkuu ama wale ambao wanahusika. Inatakikana kuwe na ule msukumo wa kumwambia ya kwamba lazima aende hospitalini ndio aweze kupata maagizo ambayo yanapaswa kufuatiliwa."
}