GET /api/v0.1/hansard/entries/1368730/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1368730,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1368730/?format=api",
    "text_counter": 305,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": "Nami pia ninapenda kuingia katika kumbukumbu za kupigia upato na kupatia Mswada ulio mbele ya Bunge hili kongole. Umeletwa na vinara wetu wa Bunge hili la taifa; Kinara wa Wengi na Kinara wa Wachache. Ninawapa hongera kwa kuleta marekebisho kidogo ili kufanya Mswada huu kuwa wa kikatiba. Mimi kama mama-kaunti wa Kwale ninafurahia pesa za NG- CDF. Ninafurahi ninapowaona Wajumbe wakiwajibika kuwafanyia miradi watu wa Kwale. Kwanza pesa ile ambayo inafanyiwa miradi inamfaidisha mwananchi wa Kwale kupunguza umaskini. Biashara inayofanywa na NG-CDF pale Kwale ni biashara ambayo imebaki katika eneo la Kwale na inafaidisha kina mama na vijana wengi sana. Mhe. Spika wa Muda, ujio wa NG-CDF kwa kusema kweli umemaliza umaskini mashinani. Wakati wa nyuma sisi tukiwa tungali tunasoma, wazazi wetu walikuwa wanatulipia karo ya shule ambapo walilipa kila kitu. Ujio wa NG-CDF ni wa maana sana. Na kupitia njia hii, wanafunzi wengi kutoka Kwale ambao wametoka familia maskini wameweza kupata elimu. Wanafunzi hao hawangeona elimu kama si ujio wa NG-CDF. Mimi ninapenda kuunga mkono marekebisho haya na pia niseme kwamba nimefurahishwa na ibara ya 19(a) ambayo inasema Waziri hawezi kumaliza kazi yake wakati ameteua board members . Lazima wataletwa katika Bunge hili waweze kupigwa msasa na Wabunge ili waweze kuidhinishwa kuweza kufanya kazi. Ninajua kwamba kama hii nafasi ingeachiwa mawaziri basi wangechagua ma-girlfriends, marafiki zao na watu wao wa karibu lakini Bunge linavyofanya kazi… Mhe. Spika wa Muda, pole. Ninajua nimekukwaza; naomba msamaha."
}