GET /api/v0.1/hansard/entries/1369373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369373,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369373/?format=api",
"text_counter": 552,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Tunajua tuna dhuluma za kihistoria za mashamba katika taifa letu. Ninaamini lazima ardhi hiyo ilikuwa ya wenyeji kabla ya EAPC kuwa na umiliki wake. Tukichakurachakura, ninajua tutagundua kwamba hawakuipata kwa njia inayostahiki. Niseme hivi: Serikali ya nyuma ilikuwa ya Mhe. Uhuru Kenyatta na Rais wa sasa alikuwa naibu wake. Kulikuwa na kesi kama hiyo kule Likoni, kesi ya shamba la Waitiki. Wakati huo, viongozi waliwaita wakaazi waliokuwa wameingia katika shamba lile la Waitiki na wakafanya mazungumzo. Walitoa fidia kiasi fulani na Serikali ikatoa fidia nyingine. Wananchi hawakufurushwa. Kwa nini wakaazi wa Mavoko walifurushwa na kukandamizwa katika haki zao za kimsingi? Jambo la pili ni kuwa tuliona Mheshimiwa Naibu wa Rais akitetea wakaazi wa Nyandarua juzi na jana. Hawa walifaa kufurushwa na shirika la reli. Alisimama kidete akasema hawatafurushwa na kwamba watafanya mazungumzo. Kwa nini wakaazi wa Mavoko The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}