GET /api/v0.1/hansard/entries/1369374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369374,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369374/?format=api",
"text_counter": 553,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "walifurushwa kwa hali ambayo si ya hadhi wala utu? Serikali ina wajibu na haki ya kupatia Wakenya makaazi na elimu. Ni vipi makaazi, shule na makanisa yatabomolewe na kuvunjwa illhali Katiba yetu inatupatia haki ya kuabudu? Kwa hakika, nimemnukuu sana Mheshimiwa Rais alipokuwa akifanya kampeni. Alisema kwamba Serikali yake haitagandamiza Mkenya kwa kumfurusha kiholela kutoka katika mashamba. Vipi sasa amepata kura, akawa baba wa Taifa la Kenya, na anagandamiza Wakenya katika hali kama hii ambayo si ya kimsingi? Tumeona akina mama na watoto wanavyopata shida. Hata kama ni kufurushwa, basi iwe kwa njia itakayolinda hadhi, heshima, maisha na usalama wa Mkenya. Swali ni: Je, kulikuwa na usalama? Hakuna. Tuliona tear gas zikirushwa kila mahali. Je, kulikuwa na hadhi? Jibu ni kwamba hakukuwa na hadhi. Vyombo vilirushwa huku na kule. Kila kitu kilikuwa kinaangushwa kila mahali na hakukuwa na hadhi yoyote iliyowekwa. Mhe. Spika wa Muda, ninataka kusema kwamba sisi tunasikitika kama taifa ikiwa EAPC sasa wanasema kuwa wanataka kuuza ile ardhi wakati wamefanya hasara kubwa kama ile na kuwatia Wakenya dhiki. Kuna Mkenya alijitoa uhai kwa sababu ya kufikiria gharama alizotumia kuwekeza kwa kujengea familia yake makazi. Jamani, sisi Wakenya! Tunazungumzia kuwapa watu makazi halafu kwa upande mwingine tunavunja makazi ambayo wamejenga kwa miaka mingi tena katika hali ngumu sana ya kuchukua loans na tunachoita"
}