GET /api/v0.1/hansard/entries/1369376/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369376,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369376/?format=api",
"text_counter": 555,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "kwa Kiingereza. Akina mama wameunda vyama ili kupata pesa. Inakuwaje katika siku moja tu, wanafanyiwa dhuluma kama hiyo? Kama Taifa la Kenya lazima tujue sheria ni msumeno, unakata mbele na nyuma. Haiwezi kuwa sheria ifanye kazi Mavoko lakini katika sehemu nyingine inachukua mkondo mwingine. Jamani leo ni Mavoko na kesho itakuwa sehemu nyingine ya Taifa la Kenya. Hawa Wakenya tutawapeleka wapi? Wakati uchumi wa Kenya in mgumu, mwananchi ana shindwa kupata chakula, kupeleka mtoto shuleni na leo anabomolewa nyumba ambayo imemgalimu karibu shilingi milioni ishirini na kwenda juu. Jamani hilo halikuwa suluhisho. Sasa wanasema watauza hayo mashamba. Kwa nini Serikali haikufikiria hivyo mwanzoni? Anayetoa stakabadhi za shamba ni nani? Ni Wizara ya Ardhi. Wizara ni nani? Ni Serikali. Kwa nini hawakujua kulikuwa na utepetevu na ufisadi kisha kufuatilia jambo hilo kabla ya kufurusha Wakenya? Wametesa akina mama na wanafunzi walioko pale. Ni masikitiko makubwa. Lazima Wakenya wasome kwa sababu wengi hawataki kuambiwa wanataka kuona. Wameona sasa Kenya Kwanza ilipowafikisha. Sisi tuliwaambia ingekuwa ni Mhe. Raila…"
}