GET /api/v0.1/hansard/entries/1369459/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369459,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369459/?format=api",
"text_counter": 638,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili pia nikemee na kulaani ubomoaji wa majumba uliofanyika Mavoko. Ni jambo la kusikitisha, kuhuzunisha na kushangaza. Mimi nimeomba kuzungumza tangu saa nane na nusu - nimebonyeza kitufe cha ombi tangu Hoja hii ikija. Lakini kwa sasa, ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Ni kwa sababu tunataka kukemea hili jambo ili lisifanyike tena sehemu nyingine nchini. Ndio sababu tunakaa kwa muda mrefu. Hata ukiweka kikao hadi saa saba tutakaa. Hili ni jambo la kusikitisha. Watoto, akina mama na wazee wametoa machozi pale. Mtoto hajui jinsi amnyamazishe babake; baba hajui iwapo amnyamazishe mtoto; na, mama hajui afanye nini. Mhe. Spika wa Muda, ninakuhakikishia kuwa hii itarudia wale wote waliohusika katika ubomoaji huo. Iko siku nao watalia kwa jambo lilo hilo. Na kama hawakulia wao, watalia wa familia yao. Watalia vizazi vyao. Lakini watalia kwa sababu wamefanya jambo la kinyama sana. Taifa ni mahali panaolinda wananchi wake. Mtu amekuja, amenunua ardhi, hakuna mtu amemuuliza. Amechimba msingi, hakuna mtu amemuuliza. Ameanza kuweka jiwe la kwanza, amekata vyumba, amemaliza paa, amevuta moto, amevuta maji, hata wamezaana hapo hapo na wamekaa kwa miaka, ndio mtu anakuja leo na kusema hapa sio kwao. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Ulikuwa wapi wakati akichimba msingi? Wengi kati ya wale watu wamechukua mikopo. Wengine wamelipwa pesa zao za uzeeni wakaenda kujenga maisha yao pale. Unawamaliza hapo hapo, na hasa ukiangalia uchumi ulivyo mbaya. Waliojenga pale walipewa stakabadhi na serikali za ugatuzi au county governments na"
}