GET /api/v0.1/hansard/entries/1369466/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369466,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369466/?format=api",
"text_counter": 645,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii na mimi niweze kupiga pondo au kuongezea Hoja iliyoko mbele ya Bunge hii. Kwa kweli, ninataka kulia pamoja na watu wa Mavoko wanavyolia. Wao ni majirani wangu. Pale Kwale nimepigiwa kura na jamii ya Wakamba walio wengi sana. Na tangu juzi, wamekuwa wanasikitika na kunipigia simu sana. Nikiwa nao katika mikutano wanauliza, ‘Mhe. ni kwa nini viongozi mnaangalia wakati watu wa Mavoko wanauwawa mkiona?’"
}