GET /api/v0.1/hansard/entries/1369470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1369470,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369470/?format=api",
    "text_counter": 649,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": "Poleni watu wa Mavoko kwa kitendo hiki. Sisi watu wa Kwale tunasimama na nyinyi, tutatia ubani ama uvumba. Tunaomba na kuuliza kama hii ni haki imewatendekea watu wa Mavoko. Mwenyezi Mungu simama na watu hawa. Pia, ninaomba Bunge hili litengeneze tume maalum ya kuweza kuagalia swala hili la Mavoko na kupitisha kwamba hawa watu walipwe. Tena walipwe vizuri na waweze kuishi maisha mazuri. Ninataka kujenga matumaini kwa hawa watu; wasivunjike moyo. Kuna kesho yenye inakuja hapa duniani, na sio kesho ya aheli. Kama ndugu zangu Waislamu wanavyosema, malipo ni kesho aheli. Tunataka malipo yawe hapa dunia ndiyo kila mtu aone. Asante sana Mhe. Naibu Spika. Ninasema poleni sana ndugu zetu wa Mavoko, tunalia na nyinyi usiku na mchana."
}