GET /api/v0.1/hansard/entries/1369611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369611,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369611/?format=api",
"text_counter": 80,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kikuyu, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kimani Ichung’wah",
"speaker": null,
"content": " Asante Mhe. Spika wa Muda. Ninataka nijiunge na Wabunge wengine kuchangia hili jambo la Barabara ya kutoka Jitoni kwenda Rabai katika Wadi ya Jomvu Kuu, Eneo Bunge la Jomvu. Hii Barabara naielewa kwa sababu inashikanisha Jomvu na Kilifi. Nilikuwa pamoja na aliyekua Naibu wa Rais, ambaye hivi sasa ndiye Rais wa Kenya, Mheshimiwa Rais William Ruto, alipoenda kuzindua ujenzi wa ile barabara katika mwaka wa 2018. Ni jambo la kushangaza kwamba barabara ambayo ujenzi wake ulianza mwezi wa tatu, mwaka wa 2018 mpaka leo haijakamilika. Ni vizuri watu wa Jomvu na watu wa Kilifi waelewe kwa sababu hii ni moja ya barabara nyingi nchini ambazo ujenzi wao ulisimamishwa makusudi eti kwa sababu zilianzishwa na aliyekua Naibu wa Rais, ambaye sasa ndiye Rais. Serikali iliyopita ilipokuwa ikisimamisha miradi hii ilikuwa ikifikiria kwamba inampunguzia umaarufu aliyekuwa Naibu wa Rais, na hiyo ni siasa duni. Siasa duni ndiyo imewaweka nyuma watu wa Jomvu, Kilifi na Wakenya wengine, wakiwemo watu wangu wa Kilifi – Hapana, siyo Kilifi. Wakiwemo watu wangu katika Eneo Bunge la Kikuyu."
}