GET /api/v0.1/hansard/entries/1369616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1369616,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369616/?format=api",
    "text_counter": 85,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kikuyu, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kimani Ichung’wah",
    "speaker": null,
    "content": " Nilikuwa ninasema hata kwangu Kikuyu ujenzi wa barabara nyingi ulisimamishwa kwa sababu zilikua zimeanzishwa na aliyekuwa Naibu wa Rais wakati huo, na waliokuwa na hatamu ya uongozi walikua wanataka eti wazime umaarufu aliokuwa nao Naibu wa Rais kwa kusimamisha miradi ya barabara na miradi mingine ya maendeleo ambayo manufaa yake ni kwa Wakenya wa kawaida. Serikali ya leo, ambayo inaongozwa na Rais Wiliam Ruto, imechukua hii miradi yote ili ihakikishe inaendelea. Rais juzi alitembea kwote duniani. Alitembelea nchi ya Uchina kuhakikisha kwamba kandarasi nyingi, ambazo zinatekelezwa na wanakandarasi kutoka Uchina, zinapata fedha ili ziendelee. Kandarasi ambazo pia zinatekelezwa na Wakenya zimejumuishwa kwenye mpango huo. Pia, hivi majuzi Rais alipokuwa nchini Ufaransa, mashirika ya IMF na World Bank The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}