GET /api/v0.1/hansard/entries/1369619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1369619,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369619/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kikuyu, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kimani Ichung’wah",
    "speaker": null,
    "content": "Ni mzito kwa maneno ya kuwatetea watu wa Jomvu ili waweze kupata maendeleo, na hiyo ndiyo sababu alichaguliwa na watu wa Jomvu. Ninajua alipitia magumu kwa sababu alikuwa anaonekana kuegemea sana upande wa Rais William Ruto. Hatahama alichosimama nacho kuwania ubunge kilikuwa kinaegemea mrengo wa Serikali ya sasa. Ninataka nikuambie, mtu wa Jomvu; endelea kusimama na kumuunga mkono Rais William Ruto, ambaye atatukamilishia miradi ya maendeleo katika eneo Bunge la Jomvu na Kenya nzima. Wacha nikupongeze kijana mwepesi, na uendelee kuwa mzito wa maneno na mzito wa maendeleo. Kuwa mzito uhakikishe kwamba ujenzi wa barabara katika eneo Bunge lako umekamilishwa. Hiyo ndio kazi watu wa Jomvu walikupa. Pongezi na kongole kwa kuleta hii petition . Hii ndiyo kazi uliyochaguliwa uje ufanye hapa Bungeni. Na usitishwe na mtu yeyote. Jana nilisikia watu fulani wakisema eti tutoe fedha za maendeleo za kukamilisha barabara kama hii tuzipeleke kwenye Hazina ya Vyama vya Kisiasa. Eti wanataka pesa za miradi ya maendeleo zipelekwe kusimamia vyama vya kisiasa kwa sababu huko ndio wanapata kitu cha kula. Uporaji wa pesa za vyama vya kisiasa ni lazima ukome. Tunataka fedha zisiende kwenye vyama vya siasa, bali ziende kwenye miundo msingi na kwenye miradi kama hii iliyokomeshwa kwa sababu ya siasa duni za hizo vyama. Asante Mhe. Spika wa Muda."
}