GET /api/v0.1/hansard/entries/1369621/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369621,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369621/?format=api",
"text_counter": 90,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ndia, UDA",
"speaker_title": "Hon. George Kariuki",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Pia, mimi ninaunga mkono hili Ombi la Mhe. Badi ambaye ni mwanakamati wa Kamatai ya Barabara na Uchukuzi. Ni Mheshimiwa shupavu na anaelewa kazi yake. Mhe. Bady ninataka kukuhakikishia wewe ukiwa Mwanakamati wa Kamati ya Barabara tutaunga mkono hili pendekezo lako na tutahakikisha hizi kilomita tatu zimebaki tumesukuma wenye wanashughulikia, na ninafikiri hii ni KURA ndio wamalize hizo kilomita tatu kwa sababu kama wamefanya kilomita kumi na mbili, tatu tunaweza kusukuma kupitia fedha zenye ziko ndio wamalizie huo mradi. Hili si jambo lenye Eneo Bunge la Mhe Bady pekee yake. Iko kila eneo Bunge la hii nchi. Ata nikikuuliza Bi. Spika wa Muda kama kuna barabara imekwama kwako utaniambia kuna barabara moja, mbili au tatu. Hata kwangu ukiniuliza niko na barabara ilikuwa ijengwe kabla ya kuingia Bunge na sasa niko katika muhula wa pili na imekwama. Inatoka mahali panapoitwa Baricho inaenda Getuya inaenda mahali panapoitwa Kagumo na imekwama. Hili ni janga linatuathiri sisi wote kama Wabunge na tuko kwa hii hali kwa sababu ya upungufu wa pesa. Mara nyingi tunapitisha bajeti hapa lakini inabidi turudi tena kukata hiyo bajeti kama tulivyofanya juzi. Tulipokuwa tukitengeneza bajeti, tulipunguza Ksh30 bilioni kutoka kwa barabara. Mhe. Spika wa Muda, ninaunga Ardhilhali hii mkono kabisa. If you allow me to switch toEnglish."
}