GET /api/v0.1/hansard/entries/1369635/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1369635,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369635/?format=api",
    "text_counter": 104,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kikuyu, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kimani Ichung’wah",
    "speaker": null,
    "content": " Hoja yangu ya nidhamu ni kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Miundo Msingi na Barabara, anadai kwamba Waziri hakuwa na haki ya kusema alivyosema jana. Ilhali anajua kwamba hakujileta hapa. Aliagizwa aje kujibu swali ambalo Mbunge wa Kathiani, Mhe. Robert Mbui alikuwa ameuliza. Tulikuwa tukifuatilia Kanuni za Bunge kwamba Mawaziri wakiitwa Bungeni, kujibu maswali ama kusema mambo yanayohusu Wizara zao ni lazima waje. Ninajua kuna maswala tata ambayo aligusia, lakini ni haki yake akijibu maswali. Kwa hivyo, ninaona Mhe. George Kariuki, Mwenyekiti wa Kamati ya Miundo Msingi na Barabara, amekosea kidogo, kwa kusema Kanuni za Bunge hazimruhusu Waziri kujibu lile swali. Bunge ndio ilimwalika na tusiweke ilani kuwa kuna Mawaziri wanaofaa ama tuweke vikwazo kuhusu yale ambayo wanafaa kusema wakijibu maswali. Lazima wakuje kujibu maswali."
}