GET /api/v0.1/hansard/entries/1369792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1369792,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369792/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Ninaunga mkono Ripoti hii na kumpongeza Mwenyekiti na kamati yake yote kwa kazi nzuri ambayo wameifanya. Itajulikana kama vile wanenaji wenzetu walivyosema juu ya haya mambo ya asset recovery ama urudishaji wa mali iliyonyakuliwa ni jambo la muhimu kukiwa kutakuwa kumewekwa sheria. Mimi nimetoka kwenye mkutano sasa hivi wa kamati yangu ya uchukuzi ambapo leo tulikuwa tumemwita Mkurugenzi wa Almashauri ya Viwanja vya Ndege wa hapa Nairobi. Yale ambayo tumeweza kuyazungumzia, tunaona kuwa kulikuwa na ardhi kubwa sana ya Almashauri ya Viwanja vya Ndege lakini ardhi ile karibu robo tatu imenyakuliwa. Hii ni kazi ambayo kamati hii na Serikali yafaa sana kuangalia kwa sababu mara ya kwanza walikuwa na sababu ya kusema walikuwa wanataka kustawisha uchumi ama biashara kwa kutengeneza godowns kisha baadaye wakabadilisha. Badala ya godowns zikakuwa ni mahoteli ambayo yanatengenezwa hapo. Na sio Nairobi peke yake. Mombasa, Kisumu na sehemu nyingi pia hali ni ile ile. Hali hii ilikithiri katika uongozi uliopita. Tunaona leo mali ya Shirika la Reli imeweza kunyakuliwa kila mahali. Tukiangalia ni sehemu ya mashirika mengi ambayo watu wamechukua na pesa hizo unaziona kama wanenaji wenzangu walivyosema, zinarudi sasa. Pesa hizo ambazo si halali zinatumika katika mambo mengine kama uchaguzi na kutafuta uongozi. Kwa hayo machache, ninachukua fursa hii kuunga Ripoti hii mkono. Ninawapatia wanenaji wenzangu nafasi pia waweze kuchangia."
}