GET /api/v0.1/hansard/entries/1369840/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369840,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369840/?format=api",
"text_counter": 309,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ugaidi umekuwa donda sugu dunia nzima. Licha ya kuwa ninaunga mkono Hoja hii, ningependa kusema kuwa sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma. Sheria za ugaidi zisitungwe tu ili kudidimiza watu fulani, ilihali wale wanaojihusisha na ugaidi wanaachwa. Tumekuwa na vijana waliopoteza maisha yao kwa kushukiwa kuwa ni magaidi. Juzi, tuliona watu zaidi ya 400 waliokufa kule Shakahola. Inasikitisha kuwa mhusika mkubwa amepewa kifungo cha mwaka mmoja peke yake, ilhali maisha ya watu yamepotea. Sisi, kama Bunge, tunatakikana tutunge sheria ambazo zitaweza kufuatwa na Serikali. Maisha mengi yalipotea pale Shakahola. Sheikh wetu, Aboud Rogo, alimiminiwa risasi nyingi sana kwa kushukiwa tu, lakini huyu mhusika mkuu wa vifo vya Shakahola ambavyo vimethibitika na kuna makaburi ya halaiki, amepewa kifungo cha mwaka mmoja tu. Mimi, kama mama wa Mombasa County ninashangaa sana!"
}