GET /api/v0.1/hansard/entries/1369842/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369842,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369842/?format=api",
"text_counter": 311,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Subiri ndugu yangu, Mheshimiwa wa Magarini. Inatakikana hizi sheria za mambo ya ugaidi zilizotungwa ziangaliwe zaidi. Nikitumia mfano wa Israeli na Palestina, mataifa haya yote yako katika Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, leo Wapalestina wanauawa na Waisraeli, na Umoja wa Mataifa umeshindwa kuwadhibiti. Tunapozungumza, Jumba hili liweke rekodi. Ikiwa mtu ameua, awe ni Muislamu au wa dini tofauti, lazima sheria ifuatwe. Kwa hivyo, isiwe ni watu fulani ndio wanalengwa katika jamii. Ikiwa mtu ni mbaya, ni mbaya tu. Ninaunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Kamati ya kudhibiti mambo ya ugaidi kwa kufuata kanuni za Umoja wa Mataifa. Mwenzangu ananitoa timing . Sipendi kuzungumza mtu akiniingia kwa akili yangu. Mheshimiwa, utapata wakati wako."
}