GET /api/v0.1/hansard/entries/1369859/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1369859,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369859/?format=api",
    "text_counter": 328,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia kama vile wenzangu walivyochangia. Kwanza, maneno ambayo nitatofautiana na rafiki yangu, Mhe. Tongoyo, ni yale maneno ambayo anasema: Kuwa mambo haya ya ugaidi yasiingizwe kwenye mambo ya kidini. Jambo hilo si jambo ambalo linatakikana kuchukuliwa asilimia mia, kwa sababu kama alivyosema Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Mombasa, Mama Mhe. Zamzam - mama wa kazi – msumeno hukata mbele na nyuma. Tukiangalia, kuna watu kama Aboud Rogo na Abubakar Shariff alias Makaburi, ambao waliuawa kwa shauku tuu, kuwa mshukiwa huyu anahusiana na mambo ya ugaidi. Abubakar Shariff alias Makaburi alitabiri kifo chake kulingana na ile hali ambayo alikuwa anafuatwa. Kama vile ilivyosemwa leo, huyo ashukiwa, lakini yuko mtu ambaye makaburi yamepatikana katika shamba lake kabisa. Mpaka leo, anabembelezwa huku, kisha kwa filamu na baadaye kufungwa kwa mwaka mmoja. Na bado kuna kesi nyingine. Hatujui pengine katika huu mwaka mmoja, anawekewa labda kitanda, televisheni na kila kitu hapo ndani. Mbona hawakuwapa nafasi hao akina Aboud Rogo na wengine kama vile ambavyo hawa wamepewa nafasi? Jambo la pili, tukiangalia hii hali ya mambo ya ugaidi, tunaona kama vile watu wanabandikiwa kuwa wanaweka ndevu kama vile mimi, Mhe. Bady… Siku hizi nimeanza kuweka ndevu na sasa pengine nitakuwa mtuhumiwa pia kulingana na hivi ninavyokaa. Ninataka kusema kitu kimoja juu ya mambo ya uhalifu na hali ya dhulma za kibinadamu. Leo hii tunaangalia Palestine. Wanaua mpaka watoto katika hospitali, nyumba na kila mahali. Udhalimu mkubwa! Halafu Netanyahu anasema ni vizuri you kill them before theygrow up! Kabla hawajakuwa, uwabatilize mapema ili wasiwe na matatizo wakati ujao."
}