GET /api/v0.1/hansard/entries/1369880/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369880,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369880/?format=api",
"text_counter": 349,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": " Hon. Temporary Speaker, I stand guided . Ninasema kwamba kulingana na hali ilivyo wakati huu, tumepoteza watu wengi. Leo, ukitembea Majengo, King’orani, Mji wa Kale na sehemu zingine katika Kaunti ya Mombasa, wazazi wanalia kwa sababu hawajui watoto wao wako wapi. Wengi wamepotea kwa sababu ya kutumiwa kufanya mambo ya ugaidi. Kama alivyosema Mhe. Tongoyo, mambo haya usiangalie dini wala rangi. Gaidi ni gaidi. Kwa hivyo, ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu ina mambo mazuri. Leo ni siku nzuri sana kwetu kama viongozi, hasa mimi, kwa sababu nimeongea kwa niaba ya watu wangu kama Mbunge wa Jomvu. Kuna kijana kutoka Jomvu aliyepotea katika Msikiti wa Musa, na mpaka wa leo hajaonekana. Familia yake, akina Rehema Karim na wengine, wakitazama taratibu za Bunge, wanajua kweli tumejaribu kuzungumzia jambo hili. Mhe. Spika nimeshukuru na ninaunga mkono Hoja hii. Na kama alivyosema Mhe. Zamzam, hatuwezi kutofautisha gaidi na watu wengine. Huwezi kumjua mtu anayeweza kukupiga risasi. Mhe. Owen, nitakutetea wakati wowote ili usipigwe risasi."
}