GET /api/v0.1/hansard/entries/1369905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1369905,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369905/?format=api",
    "text_counter": 374,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Ninaunga mkono ripoti ambayo imetolewa na Kamati hii ya Usalama. Hakuna dini, iwe ya Wakristo au Waislamu inayounga mkono ugaidi. Gaidi hana sura, rangi au kabila. Gaidi ni gaidi. Kenya imeathirika pakubwa na mambo ya ugaidi. Hivi tunavyozungumza, ndugu zetu wa Lamu wanaendelea kuumia kwa mambo ya ugaidi. Lazima sisi, kama taifa ama viongozi, tutafute chanzo au kiini cha vijana wetu kujiunga na makundi ya kigaidi. Tukipata jibu, basi tukiunda sheria itatumika kudhibiti vijana wetu ndio wasijiingize katika makundi ya kigaidi. Swala nyeti ni kwamba uhaba wa kazi hapa nchini umechangia pakubwa vijana wengi kujiingiza na makundi ya kigaidi. Hii ni kwa sababu wanashawishiwa na pesa."
}