GET /api/v0.1/hansard/entries/1369907/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369907,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369907/?format=api",
"text_counter": 376,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": "Jambo lingine ni kwamba polisi ambao wametwikwa jukumu la kuzuia ugaidi wasigeuke na kuwa magaidi. Ni lazima watumie hekima na wafanye uchunguzi thabiti kabla ya kushika mtu au kumpiga risasi. Haya si mambo ya kudhania, na wao ndio wametwikwa jukumu la uchunguzi ili wajue wahalifu. Ukisema mimi ni mhalifu, na bado hujanichunguza ujue mienendo yangu ya kihalifu ni gani, au nina husiana na akina nani, halafu unishike na kunipeleka kotini... Uchunguzi duni ndio sababu watu wengi wamepelekwa kotini na kupatikana hawana hatia."
}