GET /api/v0.1/hansard/entries/1369955/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369955,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369955/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuzungumzia uhifadhi wa Kaya yetu kama Wamijikenda. Kwanza, ninamshukuru Mhe. Owen Baya, ambaye ni jirani yangu kule Kilifi North, kwa Ombi hili ambalo amewasilisha Bungeni. Ninamuunga mkono ili tuweze kuhifadhi makao yetu kama Wamijikenda. Huo ni tamaduni yetu Wamijikenda. Ni lazima tuhifadhi sehemu kama hizo ili ziwe funzo kwetu na kwa vizazi vijavyo. Tuko na mila na tamaduni zetu kama Wamajikenda. Tukiziondoa, hatutakuwa na jambo lolote la kujivunia. Kwa hivyo, ninasimama kuliunga mkono Ombi hili. Ni lazima tuhifadhi Makaya na culture yetu kama Wamijikenda ili tuweze kusaidia vizazi vinavyokuja."
}