GET /api/v0.1/hansard/entries/1369957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1369957,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1369957/?format=api",
"text_counter": 39,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, ninamshukuru ndugu yangu, Mhe. Owen Baya, kwa kuleta Petition hii katika Bunge letu. Kaya ni sehemu moja ya desturi za Wamijikenda. Kaya ni sehemu ya msitu ambapo sisi Wamijikenda tunaenda kuomba kwa ajili ya mvua, afya njema, chakula, na amani katika taifa letu. Tunapaswa kuhifadhi misitu ya Kaya bila kuiharibu. Juzi kulikuwa na zoezi la kupanda miti nchini. Kaya hizi ni misitu mikubwa na inaweza kuhifadhiwa na kuongezwa. Ningependa tuzingatie unyakuliwaji wa baaadhi ya Kaya zetu. Manyumba ya kifahari yanajengwa huko, haswa sehemu za Kwale na Kilifi. Mambo kama haya yanaathiri utamaduni wetu kama Wamijikenda. Kwa hivyo, ninaunga mkono Ombi hili. Tuendelee kulinda misitu yetu. Pia, inapaswa itambulike na kuwekwa katika sheria kuwa ni hatia kuharibu misitu ya Kaya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}