GET /api/v0.1/hansard/entries/1370217/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1370217,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370217/?format=api",
    "text_counter": 299,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Suala la ugaidi lina utata sana. Halina dini wala kabila. Nimetoka Lamu, ambayo imekuwa katika vyombo vya habari mara nyingi kwa sababu ya mambo ya ugaidi. Wengine wamekuwa kwa vyombo vya habari kwa sababu ya utaalamu fulani, lakini sisi saa zote tukitajwa kwa habari ni kwa sababu ya mambo ya ugaidi. Eneo Bunge langu linaathirika sana na mambo ya ugaidi. Suala hili likizungumzwa, tunazungumza kutoka ndani mwa roho zetu kwa sababu ni mambo ambayo tunajua yanatuathiri. Kuna mtu mmoja ambaye ameuawa leo. Ninatoa pole zangu, kisha niendelee kuchangia Hoja hii."
}