GET /api/v0.1/hansard/entries/1370220/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1370220,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370220/?format=api",
"text_counter": 302,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Tumeteseka sana. Ninataka nizungumzie suala hili leo. Nina hofu ya kuunga au kukataa Hoja hii leo. Ikiwa ni suala la ugaidi, ni lazima nisome na nielewe. Mambo ambayo yanafanyika kule Lamu yanaleta utata na hatuyaelewi. Kuna watu ambao hutumia matukio ya ugaidi kufanya uhalifu wa wenyewe kwa wenyewe kisha uhalifu huo ukahesabika kama ugaidi. Hofu yangu kubwa ni kwamba watu wengine watatumia sheria kugandamiza jamii zingine ili ziitwe magaidi. Kuna utata kule Lamu. Kuna watu ambao wameuwawa kwa sababu ya biashara, au kutopendwa na ikasemekana kuwa huo ni ugaidi. Haya mambo yanafanyika na tunajua watu ambao wameuwawa na ikasemekana kuwa wao ni magaidi ilhali si magaidi. Huwa inapatikana kuwa kuna mtu ambaye anataka shamba lake au anashindana naye kwa sababu ya mafuta na mambo mengine."
}