GET /api/v0.1/hansard/entries/1370222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1370222,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370222/?format=api",
"text_counter": 304,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Jamii zingine zimehamia katika eneo hilo na kuendelea kuwa wengi hadi wakawa na kiburi na kusema kuwa watachukua viti vyote katika uchaguzi. Ninataka Serikali ichunguze suala la magaidi kwa sababu kuna mambo ambayo yamefanyika na watu wanajificha kwenye ugaidi. Kwa mfano, ningependa kuzungumzia jambo ambalo Wakenya hawalijui. Ningependa kulieleza hapa ili walijue. Kuna kanisa iliyochomwa, jambo ambalo lilileta vita kati ya Wakristo na Waislamu. Kuna watu ambao wanafaidika wanapowagombanisha Wabajuni au wakaazi wa Lamu na jamii zingine. Wanataka kuzidisha ugomvi wa kidini ili mtu ajinufaishe kisiasa."
}