GET /api/v0.1/hansard/entries/1370321/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1370321,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370321/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza ningependa kuwatakia watu wote katika Bunge hili, hasa Maseneta wenzangu, mwaka mpya wenye heri. Tumetoka likizo ndefu. Mashinani tumeonana na wananchi. Tumetatua zilizokuwa katika kaunti zetu. Pili, hawa waliyochaguliwa katika Kamati hii ya SBC ni Maseneta ambao wamebobea sana katika kazi zao. Mawakili wako humo ndani na wengine ambao ni Maseneta waliobobea katika nyanja mbalimbali. Kwa hivyo, nina imani ya kwamba katika kipindi hiki ambacho tumeingia sasa hivi, tutaweza kujadili mambo mengi sana ambayo yataweza kutusaidia na kufanikisha watu wetu hususan katika mambo ya gatuzi. Ninawasihi Maseneta wenzangu, tuweze kuhudhuria vikao kwa wingi sana katika kipindi hiki ili tuyatekeleze majukumu yetu makubwa kama Maseneta. Tuweze kujumuika kusaidia kaunti zetu na kuhakikisha ya kwamba tunaleta Miswada muhimu sana ambayo itasaidia kaunti zetu. Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa ninaunga mkono Hoja hii."
}