GET /api/v0.1/hansard/entries/1370362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1370362,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370362/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuwasabahi Maseneta wenzangu. Pili, namshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuvuka mwaka. Natumahi kwamba mwaka huu utakuwa wa ufanisi. Langu ni kuhimiza Seneti na kuomba kwamba mwaka huu uwe wa mabadiliko katika utunzi wetu wa sheria. Wakulima humu nchini wanatarajia Seneti kupitisha Miswada na Sheria ambazo zitawawezesha kunufaika kutokana na jasho lao. Vile vile, walimu katika nchi ya Kenya wanatazamia Seneti kusimama nao na kuhakikisha kwamba mfumo wa elimu na masilahi yao pamoja na wanafunzi yanapewa kipaumbele. Mwaka uliopita tulikuwa na mchakato ungedhani ni mashine ya kusaga unga na wengi wa Maseneta walikuwa wanapiga tingatinga. Naomba tubadilishe mfumo ili Wakenya wanufaike na sheria na chochote tunachofanya hapa Seneti. Changamoto za manaibu wa magavana ni donda sugu katika kaunti za Trans Nzoia, Kisii na maeneo mengi humu nchini. Lazima Seneti itunge sheria kuhakikisha kwamba gavana na naibu wake ni kama chanda na pete. Iwapo mtu atachoka na naibu wake, wote wanafaa kufunga virago na kwenda nyumbani. Haiwezekani mmoja akishapata mamlaka, anamgeuka mwenziwe kwa sababu ameona kitita cha fedha. Naomba Seneti isimame, itambulike na ionekane kwamba italinda na kuhakikisha kwamba ugatuzi unatambulika kote nchini. Mwisho, mimi kama kijana kiongozi chipukizi, ni kuomba Seneti isimamame na vijana wa nchi ya Kenya."
}