GET /api/v0.1/hansard/entries/1370372/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1370372,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370372/?format=api",
    "text_counter": 116,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii ili niweze kuunga mkono kamati ambayo imeundwa kusimamia mipango ya Bunge hili. Pili Bw. Spika, ningependa pia kutuma salamu zangu za rambirambi kwa familia ya kijana ambaye siye wa Bonde la Ufa pekee, bali aliweza kupeperusha bendera ya Taifa letu la Kenya. Kwa sababu ni kijana wa miaka 24, ningefurahi zaidi kama ningeona kwamba bendera ya Kenya, leo hii inapeperushwa nusu mlingoti kwa heshima yake. Seneta mwenzangu Sen. Dullo amejadilia maswala ya kubuniwa kwa kamati ya kuangalia implementation ya yale ambayo tunayapitisha katika ripoti zetu. Mwaka ulipopinduka, niliweza kumpigia simu Katibu wa Bunge hili Bw. Nyegenye na nikaomba kuweza kuonyeshwa njia ya mimi kuleta Mswada ili Kamati hiyo iweze kubuniwa tena. Hii ni kwa sababu niliarifiwa kwamba katika Bunge la Pili la 2013, Kamati kama hiyo ilikuwepo na mwenyekiti wake alikuwa Sen. James Orengo ambaye leo hii ni gavana. Miongoni mwa sababu zangu za kuomba Bunge hili liweze kurejesha kamati kama hiyo ni kwa sababu ya ripoti kama ile ya Buxton Estate. Tulifanya mapendekezo yeweze kuregesha wale waliokuwa wakaazi wa eneo lile. Kwa sababu sheria imetufunga mkono, hatuwezi kufuatillia zaidi ya mapendekezo ambayo tumetoa."
}