GET /api/v0.1/hansard/entries/1370374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1370374,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370374/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa hivyo, ningependa sana utakapokuja Mswada kama ule, muweze kuniunga mkono ili tuweze kuunda kamati ya kufuatilia zile ripoti ambazo tunaziandika katika Bunge hili. Jambo la tatu, Bw. Spika, ukiweza kuangalia Bunge hili, utaona karibu kina mama sote tumevaa nguo nyeusi. Tumevaa hizi nguo nyeusi tukiashiria kusimama na yale mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa yakipiga kelele kuhusiana na wale watoto wa kike ambao wameuliwa kiholela holela kwa sababu ni wanawake. Kauli yangu mbiu ni kwa vijana na wazee, kuwambia kwamba sisi wanawake kweli tuna mapungufu yetu kama wananadamu, lakini mtoto wa kike hapigwi hata kuuwawa. Ukitaka kupiga mtoto wa kike, nunua kanga umupige na upande wa ganga. Bw. Spika, inawezekana kweli kuna makosa ya hapa na pale lakini haimaanishi uweze kuangamiza na kumaliza maisha ya mtoto wa kike. Kwa hivyo, ningependa ndungu zangu Maseneta wa kiume, muweze kusimama na sisi. Hii ni kwa sababu ukifuga nyoka, leo atauwa mtoto wa kike na kesho atakuja pia atauwa mtoto wa kiume. Kwa hayo mengi Bw. Spika, asante na niwatakie heri na fanaka za mwaka huu 2024. Ninawashukuru pia wale vigogo walionitangulia kwa kuweza kunishika mkono hadi kupendekeza Miswada mitatu, ambayo moja wao uko katika Kusomwa mara ya pili. Mswada wa kumsimamia mtoto wa kike arudi shule utaondosha nchi yetu katika umasikini. Hii ni kwa sababu itampa fursa yule mtoto ambaye ametelekezwa katika masomo yake kupata fursa ya pili kuondosha uchochole katika jamii yake. Kwa hivyo, nawaomba muweze kupitisha Mswada wa The Care and Protection of Child Parents Bill, 2023. Asanteni sana na Mwenyezi Mungu awabariki."
}