GET /api/v0.1/hansard/entries/1370380/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1370380,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370380/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, naungana na wenzangu kutuma risala zangu za rambirambi kwa familia ya mwanariadha Kelvin Kiptum ambaye aliaga dunia. Naunga mkono Mswada huu wa Kamati ya Shughuli katika Bunge kwa sababu hawa Maseneta ni wale tu ambao walikuwa kwa hii Kamati wakati ule mwingine. Kwa hivyo, ni watu ambao wako na ujuzi kwa mambo ya hii kamati. Bw. Spika, nimemsikiza Sen. Mungatana akisema ya kwamba ni vizuri tuwe na kamati ambayo itakuwa ikitekeleza mapendekezo ambayo yameletwa na kamati zingine. Naona hilo ni jambo nzuri kwa sababu mapendekezo yanayoletwa na kamati, na siyo kamati tu lakini hata na Bunge hili, yanabaki kuwa tu ni mapendekezo ambayo hayashughulikiwi. Kwa hiyo nakubaliana na yeye. Kwa sababu wakati huu tumeanza vizuri, pengine itakuwa jambo nzuri likishughulikiwa. Itaonekana kuwa katika Seneti sio tu mapendekezo tunafanya bali vilevile tunayatekeleza yale mapendekezo. Bw. Spika, vilevile nachukua fursa hii kuwatakia maseneta wote pamoja na watu wa Laikipia mwaka mpya wenye mafanikio. Naungana na Maseneta kukutakia pia wewe, Bw. Spika, mwaka mpya ulio na mafanikio. Nashukuru."
}