GET /api/v0.1/hansard/entries/1370389/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1370389,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370389/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kidogo, tunajua mwaka huu wataongeza na tutafanya kazi pamoja nao. Pili, naunga mkono Spika wetu, Maseneta wote na pia Clerk pamoja na wafanyakazi wake kwa ile kazi mlioifanya mwaka jana. Ninahakika kuwa mwaka huu tutafanya kazi pamoja ili tuweze kubadilisha nchi yetu ya Kenya. Tunajua kama Maseneta huwa tunazungumza juu ya devolution. Zile pesa tulizopatia magavana mwaka jana, wakati tulienda mashinani tuligundua kwamba ni kama kulikuwa na shida nyingi sana. Mwaka huu, ningeomba tuweze kuangalia vile Kaunti nyingi zitaongezewa pesa za elimu, afya, ukulima na idara zingine. Pili, tumeskia ya kwamba kuna naibu gavana ambaye ametimuliwa. Hii ni kama mwaka jana tuliposikia kwamba naibu gavana wa Kaunti ya Kisumu ametimuliwa. Ningeomba ya kwamba, wale watu ambao wataenda kuangalia haya mambo, wayaangalie kwa njia inayofaa. Hii ni kwa sababu, tunajua ya kwamba ni gavana ndiye ambaye anashughulika na mambo ya pesa, itakuwaje naibu wake ndiye anatimuliwa. Mwisho ni kuhusu pombe na dawa za kulevya. Watu wengi katika nchi hii wamechukua maisha yao. Vijana wetu wamepotea na kazi yao ni kukunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya. Hii ndio maana nchi yetu inaendelea kuzorota. Ningependa kuwakumbusha kuwa, wiki jana kule Kirinyaga, vijana wetu na akina mama walifariki kwa ajili ya pombe haramu. Kwa hivyo, Seneti ikipitisha pesa mwaka huu, ningeomba tuweze kutenga pesa kwa kila Kaunti kwa ajili ya kuelimisha hao watu. Asante sana. Ninaunga mkono. Mimi ni Seneta wa Embu Kaunti, naibu wa mwenyekiti wa Democratic Party."
}