GET /api/v0.1/hansard/entries/1370535/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1370535,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370535/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Naunga mkono hii Taarifa ambayo imeletwa na Sen. Oketch Gicheru, kuhusu uhusiano katika utawala wa ufalme wa Morocco na Kenya. Ni jambo la muhimu sana kuona kwamba Kenya itakuwa na uhusiano mwema na mataifa mengine. Uhusiano kama huo hua na mazao mengi. Kwa mfano, hufungua njia za watu kupata kazi na biashara. Uhusiano mwema hua unaleta mambo ya biashara kuendelea katika nchi zetu za Afrika, hususan, uhusiano baina ya Kenya na Usultan wa Morocco. Nilikua katika Bunge la Pan-African Parliament. Katika Bunge hilo, nchi ambayo imetambuliwa na Pan-African Parliament inaitwa Western Sahara. Nchi ya Morocco bado haijakua na ubalozi ndani ya Kenya. Hivi sasa kuna msikizo unaoendelea ya kwamba kuna nia ya kua na uhusiano mwema na serikali ya Morocco pia. Hilo ni jambo nzuri na tunaliunga mkono. Hata hivyo, kama kutakuwa na uhusiano kama huo, ni lazima iwe baina na ifanywe wazi kabisa ili kila mtu ajue kinachoenedelea baina ya majadiliano yanayoendelea katika Kenya na Serkali ya Morocco. Hivi Juzi tumeona majibizano ambayo yalikua hayafai. Hili Bunge la Seneti lina uwezo wa kujadiliana kuhusu jambo lolote ambalo linaendelea ndani ya Kenya. Hili Bunge likiwa linaongozwa na Spika lina uwezo wa kujadili mambo. Katika kujadiliana, unaweza ukaenda katika nyanja zozote za biashara, za kazi, matumizi, madakatari, na kila kitu ili kusaidia nchi."
}