GET /api/v0.1/hansard/entries/1370537/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1370537,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370537/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Kulingana na Katiba, hauwezi kushusha hadhi ya Bunge hili. Lakini juzi tumepata afisa mmoja anayefanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje anayeitwa Katibu wa Kudumu ambaye ni SingOei. Ni jambo la aibu kuona ya kwamba afisa wa Serikali anaweza kuingilia jambo ambalo linajadiliwa ndani ya Bunge ama anaweza kuingilia Spika ambaye ndiye kilele au mkubwa ndani ya Bunge la Seneti. Tunaona hii ni madharau na anajaribu kushukisha heshima ya Bunge la Seneti chini, ambayo sio kawaida. Wewe ukiwa unafanya kazi ndani ya Serikali hauwezi kuingilia chochote ndani ya Bunge la Seneti. Bw. Spika, tunaona haya ni matusi na madharau, haswa kwangu. Itakuwa jambo la kusikitisha sana kuona kuwa kutakuwa na madharau kama haya. Sisi kama watu wa Pwani hatutakubali hata kidogo kuona ya kwamba, sio kwamba wewe uko pale pekee yake lakini mtu yeyote ambaye anaketi katika kiti cha Uspika wa Seneti, lazima aheshimiwe. Hivi sasa, ikiwa jambo kama hilo limetendeka, ni muhimu ile kamati husika katika Seneti kuweza kumuita huyo afisa aje ndani ya Bunge hili la Seneti na kutueleza ni kwa sababu gani alikuwa anajibishana na Spika, tena anaenda kwa Twitter . Hiyo ni madharau ya namna gani."
}